 Primary Format :
Language :
Also Listed as:
City : State/Province : Country : Region : User Tags:
User Votes:
RSS Feed Website
People found this Podcast
Searching for:
View this Podcast on a Google Map. 

Text Only listing of Sauti ya Mwanakijiji Podcasts
Methings.com listings of Sauti ya Mwanakijiji Podcasts
If you like this podcast, you might also like:
|
CCM matatani; Upinzani Mashakani - ngoma 2010! Sijui kama kweli tunataka mabadiliko au tunaombea mabadiliko yatokee. Sijui kama tunafanya ili kusababisha mabadiliko au tunasubiri wengine wafanye ili tufurahie mabadiliko; Sijui hata kama tunajua vizuri ni mabadiliko gani hasa tunayataka na kama tunataka ni juhudi gani tumezifanya kushiriki kwenye mchakato wa kuleta mabadiliko hayo.
Tunaweza kubishana vijiweni na kwenye mitandao na kujaribu kubadilishana mawazo mchana kutwa na usiku kucha lakini mabadiliko hayaji kwa kusema. Mabadiliko h ... Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Ripoti juu ya Meremeta yatokaUnaweza kupata sneak ripoti hiyo kwenye http://www.mwanakijiji.com
Password ya kufungulia Ripoti Sneek Pek: meremeta1997
Inapatikana hivi: (Tafadhali angalia masahihisho kutoka taarifa yetu ya Ijumaa)
Ripoti inapatikana kwa njia ya pre-ordering (yaani order zikishatimia zote zinatolewa kwa wakati mmoja) kwa wale ambao watachangia dola 30 au shilingi elfu thelathini tu au zaidi kwa njia zifuatazo:
* Kupitia Mtandao wa http://www.mwanakijiji.com kuna kitufye cha kuchangia upande wa kul ... Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Ziara ya Dowans HQ in Costa Rica na Meremeta Hi everyone; I'm back, wounded and limping but still kicking LOL. With some of my "little ones" we were able to travel extensively through Europe, US and Costa Rica as well as making some contacts in Singapore, U.A.E (this was published in one of previous Cheche editions. What we have discovered is nothing less than shocking!
I visited the so called Headquarters of Dowans S.A in Costa Rica and had access to relevant organs that deal with businesses there. Some of the things we were abl ... Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Taarifa ya Habari Juni 10, 2009Ifuatayo ni taarifa ya habari ya saa mbili za Usiku Juni 10, 2009 kwenye TBCListen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Uvamizi na Uharibifu Arumeru: Mahojiano na Mhe. KimaroKwa usiku kucha kundi la wahuni waliojibatiza jina la "wanakijiji" na kutuchafua wengine walivamia eneo la Mhe. Aloyce Kimaro (Vunjo-CCM) na kuharibu mazao na kuchoma nyumba na kuiba mali mbalimbali, walifanya hivyo kwa kile ambacho gazeti la Mwananchi limeelezea kuwa "wanadai kwamba, kwa kuwa shamba hilo liko katika eneo lao wangepewa ili walitumie kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kujenga shule, hivyo kitendo cha serikali kuliuza kwa mtu wa nje ya kijiji hicho ni kunyanganya haki yao."
Kit ... Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Maoni yangu Juu ya Busanda kwenye Star TVSiku ya Jumamosi nilialikwa kuwa mmoja wa wachangiaji katika kipindi cha "Tulonge Asubuhi" kinachorushwa na Star TV Jijini Mwanza. Mada kuu ilikuwa tulilojifunza kutokana na Uchaguzi mdogo wa Busanda.
Wachangiaji wengine ambao nao walipata nafasi ya kuchangia kwenye onesho hilo la asubuhi ni pamoja na Erasto Tumbo (Chadema), na Amos Makalla (CCM) pamoja na wapiga simu wengine.
Ni matumaini nitaendelea kupata nafasi kama hii ili kuendelea kuchochea mabadiliko ya kifikra ambayo mara zote ... Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Kule tulikotoka, ndiko kule kwa Chinova?Unaweza kusikiliza kwa kudownload kutoka hapa au kusikiliza moja kwa moja kwa kubonyeza "play" chini hapa.
http://www.box.net/shared/qfp38sfr3n
Ukisikiliza usiniulize, na wala usimwambie mtu mwingine. For your Ears Alone!
M.M.Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Uongozi na Maendeleo: - Sauti kutoka AheraNingeweza kukuambia kilichomo lakini sitakutendea haki; itabidi usikilize mwenyewe. Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Nani ashinde, nani ataamua mshindi?Ni mgongano wa kihistoria ambao ulipaswa kutokea. Ni mgongano ambao hutokea mahali popote panapokuwa na tofauti kubwa kati ya watawala na watawaliwa. Ndivyo ilivyokuwa kwenye Mapinduzi ya Ufaransa, Mapinduzi ya Marekani na Mapinduzi ya Bolshevik (Urusi).
Ni yale yale yaliyotokea na kusababisha mapinduzi ya Cuba yaliyomuingiza Castro madarakani. Ndiyo! Ni yale yale yaliyotokea pia kwenye mapinduzi ya Zanzibar!
Migongano ya namna hiyo asili yake mara zote ni pale wananchi wanapotambua kuwa ... Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Mlipuko 511KJ Mbagala: Majanga na kuishi kwa kudra!Kwa namna fulani tunaamini kuwa sisi tuna upendeleo wa aina fulani kwa Mwenyezi Mungu, kwamba nchi yetu kwa sababu upendeleo wa pekee basi haitapata majanga. Hatujajifunza kwa ajali zinazotea mara kwa mara za mabasi, hatujajifunza kwenye ajali za majini, hatujajifunza kwenye milipuko ya mabomu na kwa hakika tuko kama tumepigwa ganzi ya aina fulani hivi.
Pamoja na kutoa pole na rambirambi, ni lazima tujiulize tutaendelea mpaka kulini kwa kutegemea rehema za Mungu? Sitoshangaa leo tutaambiw ... Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Mahojiano na Mhe. Lucas Selelii (Nzega) - "Mmekula hamshibi?"Salaam,
Tumepata nafasi ya kuzungumza kwa kirefu na Mhe. Lucas Selelii Mbunge wa Nzega, miongoni mwa wabunge wenye msimamo wa kimabadiliko na miongoni mwa vinara wa vita dhidi ya ufisadi ndani ya CCM na katika Taifa.
Tafadhali hakikisha unasoma sehemu ya ahadi yetu kwani tuna ujumbe muhimu kwa wasomaji wetu na wanachama wetu. Ungana nasi pia kwenye mijadala motomoto kwenye forum yetu ya http://www.mwanakijiji.com ambapo mojawapo ya mijadala ya kina ni suala la Rais wa zamani Mzee Ally Ha ... Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Mahojiano na Mhe. William Ngeleja kuhusu DowansMpango wa serikali kutaka kuyanunua majenereta ya kuzalisha umeme ambayo yaliletwa nchini na Kampuni ya Dowans katika mkataba wake na kampuni feki iliyoumbuliwa ya Richmond hautokani na kulazimika kufanya hivyo bali hali halisi ya hali ya nishati nchini ndiyo inalazimisha serikali kupanga kuchukua hatua hiyo. Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati na Madini Mhe. William Ngeleja alipozungumza na tovuti hii hapo jana kuelezea kile ambacho kinaonekana mgongano wa kimtazamo kati ya Wizara, kamati ... Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Kwanini Masha bado Waziri? Natamani ningeweza kusema kwa nguvu ninachosema kisema hapa. Natamani ningekuwa na sauti kubwa zaidi kuweza kusikika kuhusu mauaji ya Leticia Bahati siku tatu zilizopita. Ninachojiuliza ni kwanini Masha bado ni Waziri wa Mambo ya Ndani? Lakini kuna maswali makubwa zaidi ya hilo ambayo ninayauliza leo kwenye "Nguvu ya Hoja"! Sikiliza. Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Pinda aangusha kilio, akwepa kujibu swali! Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda ametumia nafasi yake ya kujibu maswali Bungeni kugusa hisia za wabunge kwa kuonesha uchungu uliomgusa kufuatia mauaji ya maalbino ambayo yamekuwa yakiendelea nchini.
WM Pinda alimwaga machozi hayo baada ya kuulizwa kuhusu kufafanua kauli yake iliyotaka watu watakaoshukiwa au kutuhumiwa mauaji ya albino na wao kuuawa hapo hapo. Alipoulizwa kwanini ahalalishe mauaji hayo na kwanini atoe kauli zinazonesha kukikanzina na utawala wa sheria na Katiba ambao ni msin ... Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Mwakyembe aunguruma "Mashtaka yanayoletwa ni mepesi"Mbunge wa Kyela na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Mhe. Dr. Harrison Mwakyembe amesema kuwa mashtaka mbalimbali yanayoletwa hivi sasa dhidi ya watuhumiwa mbalimbali wa ufisadi bado ni "mepesi" na anatajia kuwa baada ya uchunguzi kufanyika zaidi mashtaka hayo yatabadilishwa na kuwa mazito yakiwemo yale ya sheria ya Uhujumu uchumi.Hayo na mengine mengi ameyasema katika mahojiano yake na KLHN ya mwanakijiji.com ambayo yalirushwa moja kwa moja siku ya Jumapili. Unaweza kuyasikiliza ma ... Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Utetezi wangu wa Sofia SimbaNikiri ya kwamba nimesikitishwa na kushangazwa sana na baadhi ya ukosoaji wa Mhe. Simba kufuatia mahojiano yangu naye siku chache zilizopita. Kilichonisikitisha zaidi ni jinsi gani baadhi yetu tuna angalia vitu ambavyo si vya msingi na kuviacha vya msingi; kilichonishangaza zaidi ni jinsi gani wengine wamekuwa wa kali kiasi cha wao wenyewe kuwa kile wanachomtuhumu Mhe. Simba.. arrogance!
Katika mahojiano yangu na watu mbalimbali (kama Dr. Migiro, Dr. Salim, na wengineo) sijawahi kujaribu ... Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Mahojiano na Mhe. Sofia SimbaMojawapo ya chaguzi ambazo zimekuwa na mvuto wa muda mrefu ndani ya CCM ni ule uliofanyika mwishoni mwa juma lililopita ambapo Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM (T) alipatikana.
Mshindi huyo si mwingine bali Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe. Sofia Simba. Safari ya ushindi wake ilikuwa ni safari ambayo wachache wako tayari kuipitia. Ilikuwa ni safari ambayo unapofika mwisho inabidi ujiuliza ulianzaje safari hiyo.
Hivyo KLHN ilipata nafasi ya kuzungumza naye kwa kirefu kuhusu ... Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Exclusive: Dr. Slaa azungumzia yaliyojiri Mbeya VijijiniMwishoni mwa mwaka jana nilipata nafasi ya kuzungumza na Bongoradio.com kuhusu masuala mbalimbali ya kufunga mwaka. Ninawaletea sehemu kidogo ya mahojiano hayo pamoja na mahojiano niliyoyafanya na Mhe. Dr. Wilbroad Slaa (Karatu-Chadema) kuhusu kilichosababisha mgombea wao msomi mwanasheria Bw. Sambwee Shitambala kushindwa kufuata taratibu rahisi za kuapa kabla ya kushirki uchaguzi huo mdogo. Baada ya kusikiliza mahojiano hayo piga kura na upande wa kulia wa tovuti hii na utoe maoni yako ni ... Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Mwaka 2008: Mwaka watawala walipopigishwa magoti!Mwaka wa 2008 ndiyo huo umefikia ukingoni. Na pamoja nao ni matamu na machungu yote, furaha na huzuni, kicheko na kilio! Ni mwaka ambao umeweka historia nyingi katika nchi yetu na nje ya nchi! Hata hivyo ya nchi nyingine tutawaachia wengine, lakini kwetu sisi wenyewe tunaweza kusema pasipo shaka yoyote ile kuwa mwaka huu ulioisha ni mwaka ambapo watawala walipigishwa magoti na watawaliwa!
Jinsi gani unaweza kuuliza; sikiliza tafakari yangu ya kufunga mwaka 2008.
Nakutakia wewe na vyote ... Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Tutaka kujitawala au tulibadilisha watawala? Tulipodai haki yetu ya kuwa watu huru tulidai ili baadaye kiwe nini? Tulipoona fahari bendera ya Ufalme wa Uingereza ikiteremka taratibu usiku ule wa kukumbukwa na ya Tanganyika huru ikapindishwa tulikuwa tuna njozi ya aina gani ya Taifa? Siku ile wazee wetu walipocheza kwa furaha na kushangilia kuwa "na sisi ni huru" walikuwa wanafurahia uhuru hasa kutoka kitu nani na kwa nini?
Je yawezekana kile tulichoshangilia wakati ule, miaka 47 iliyopita sicho ambacho tunacho leo hii? Je njozi zile ... Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Julius Mtatiro azungumzia kukamatwa na Polisi kwa Uchochezi!Mara baada ya kupata dhamana katika kesi yake ya uchochezi iliyofunguliwa mjini Dar, Bw. Julius Mtatiro alipata nafasi ya kuzungumza nasi kupitia KLHN kwa kirefu kuhusu sakata zima la kukamatwa kwake na madai mbalimbali yaliyozunguka tukio la kukamatwa na muda aliokuwa mikononi mwa Polisi. Je ni kweli aliteswa, Je alikataliwa mwanasheria, na je anahusika vipi na migomo inayoendelea kiasi cha kufunguliwa mashtaka mazito kama haya?
Sikiliza majibu kupitia MWANAKIJIJI.COM au KLHN (site zote m ... Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Remembering Mama Africa Miriam Makeba - MalaikaSouth African singing legend and activist "Mama Africa" Miriam Makeba's great grandchild Lindelane (L) says farewell to her after her coffin arrived at Johannesburg's OR Tambo Airport from Italy, where she died age 76. South African President Kgalema Motlanthe on Wednesday declared a period of national mourning for music legend and anti-apartheid activist Makeba.
(AFP/DFA/Jacoline Prinsloo)
Join us at: http://www.mwanakijiji.comListen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Taarifa ya Maendeleo ya msiba wa Ndali NzaroKwa heshima kubwa na Taadhima wana Familia ya Nzaro waliopo Detroit Michigan wakiongozwa na Da Mboja Nzaro na Mwamvita Nzaro pamoja na rafiki wa kike wa Marehemu Saada Ali, wanapenda kutoa shukrani za dhati kabisa kwa niaba ya familia nzima ya Nzaro iliyoko nyumbani Tanzania pamoja na jamaa na ndugu wote kwa mwitikio mkubwa kutoka sehemu mbalimbali wa rambirambi, maneno ya faraja na misaada ya hali na mali iliyotolewa mpaka sasa.
Tunashukuru vyombo mbalimbali vya habari na hasa mitandao mb ... Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Serikali yaipiga mkwara Mwanahalisi, Kubenea ajibu hoja!Kwenye ukurasa wa mbele kuna habari iliyozua kasheshe Tanzania. Habari hii ilitoka kwenye gazeti la Mwanahalisi la Jumatano la kupokelewa kwake kumekuwa na hisia za aina yake kwani siku ya pili yake Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo iliandika barua kwa Mwanahalisi kutaka maelezo juu ya habari hiyo ambayo kwa maoni ya serikali inaonekana ni kiuchochezi na kiuchonganishi. Watu wa serikali wanaona kuwa habari hiyo ilikuwa na lengo la kumchonganisha Rais na viongozi wenzake wa CCM hasa Mhe ... Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Juu ya vifo vya Watoto 20 Tabora, siku ya Idi Mosi. Bila ya shaka utakuwa umeshasikia na kugushwa na habari za vifo vya watoto wapatao ishirini waliokuwa siku ya Idi huko Tabora kwenye ukumbi wa Muziki kutokana na kukosa hewa na kukanyagana wakitafuta kutoka ukumbini humo. Hii ni sehemu ya kwanza ya maoni yangu, sehemu ya pili itakuwa kwenye gazeti siku ya Jumapili. Ni lazima tukasirike.Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Mahojiano na Nape Nnauye kuhusu kusimamishwa UanachamaNape Nnauye ni mgombea wa nafasi ya Uenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM). Nafasi hiyo inagombewa na vijana wengine 27. Miezi michache iliyopoita Bw. Nnauye alianzisha mjadala mkubwa pale alipodai hadharani kuwa taratibu za kuingia mkataba wa Jengo la Umoja wa vijana zilikiukwa na mkataba wenye haukuwa na faida kwa umoja wa vijana. Akasema hadharani kuwa aliyewahi kuwa Waziri Mkuu Bw. Edward Lowassa pamoja na Uongozi wa Umoja huo akiwemo Mwenyekiti wa sasa Bw. Nchi ... Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Cheche mitaani Septemba 2Toleo jipya la "Cheche za Fikra" liko mitaani. Jipatie nakala yako kupitia http://www.klhnews.com Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Leo ni Siku ya Bajeti - Jisomee kabla ya kusikia!Leo ni siku ya Bajeti. Waziri wa Fedha Bw. Mustafa Mkullo anatarajiwa kusoma bajeti hiyo leo na hivyo kuonesha ni wapi tumefika toka mwaka uliopita na wapi tunataka kwenda katika mwaka ujao wa fedha.
Nimepata nafasi ya kupata nakala ya bajeti hiyo ambayo inapatikana hapa: http://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=1680&d=1213211256
Tafadhali copy and paste kwenye browser yako.
Nimatumaini yangu mtapata nafasi ya kuipitia kabla hamjaisikia.
Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Huu si wakati wa kukata tamaa! Bila ya shaka mlolongo wa matukio kadha wa kadha unaweza kumfanya mtu yeyote kushika tama na kukata tamaa. Hasa inapotokea matukio ambayo yanaihusu nchi yetu. Msururu wa kashfa ambazo zimeiandama nchi na viongozi wetu bila ya shaka vinaweza kukufanya ujisikie mpweke na mnyonge na zaidi kuweza kujiuliza "Tanzania ina matatizo gani?".
Kwa wengine kujiuliza swali hili kunaendana na hisia ya kuachwa peke (abandonment) na kukata tamaa (despair). Na zaidi ya yote kuna wengine ambao wanaweza kuj ... Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Exclusive: Mhe. Anne Kilango Malecela azungumza na KLHNTulikokuwa tunaenda siko, tumeamua kugeuka" - hayo ni baadhi ya maneno ya Mhe. Anne Kilango Malecela akizungumza na KLH News siku chache zilizopita akielezea mabadiliko ya wabunge wa CCM linapokuja suala la kulinda maslahi ya Taifa.
Kati ya mambo ambayo anayazungumzia ni pamoja na hali ya kisiasa nchini, kifo cha Ballali, kwanini wabunge wa CCM walikuwa wanaitetea serikali yao hata ilipokuwa inaharibu, kwanini anaamini Kikwete ni kweli anataka mabadiliko na ... Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Gov. Balali Afariki DuniaAliyewahi kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dr. Daud Balali amefariki dunia. Habari ambazo zimeanza kusikika tangu jana jioni na kuthibitishwa na ndugu zake zimesema kuwa Gavana Balali amefariki mwishoni mwa juma na mipango ya mazishi inafanywa. Anatarajiwa kuzikwa huko huko Marekani. Inatarajiwa taarifa ya kifo chake kutangazwa Tanzania baadaye leo. Sikiliza matangazo kuhusu kifo hicho hapa au kwa kutwa nzima ya kesho tutakuwa tunaleta maendeleo yoyote ya habari hii kwenye tovuti yetu y ... Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Alichozungumza Mhe Zitto Detroit! Karibu wiki moja iliyopita Mhe. Zitto Kabwe alizungumza na jumuiya ya Watanzania waishio Jimbo la Michigan nchini Marekani. Mazungumzo hayo yaliyofanyika wakati wa hafla ya chakula cha jioni aliyoandaliwa Bw. Zitto yaligusia mambo mbalimbali na hasa kuwataarifu wanajumuiya hiyo mambo mbalimbali yanayoendelea nyumbani na pia kusikiliza maoni na maswali yao.
Matangazo ya leo basi ni hotuba ya Mhe. Zitto kwa jumuiya hiyo na sehemu ya maswali na majibu, yote ni uncut and an edited. Makosa meng ... Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Nimevunja Mwiko - Soma "Kulikoni" la LeoKwa karibu wiki mbili sasa nimekuwa nikitengeneza hoja na kumulika kama vile kurunzi idara ya Usalama wa Taifa. Sikiliza introduction ya makala yangu maalum kwenye gazeti la "Kulikoni" leo. Kwa wale ambao hampo nyumbani makala hii itawekwa baadaye mchana wa Ijumaa (saa za Marekani) kwenye http://www.klhnews.com upande wa editorial. Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Chenge - mbona anatuchengua!?Chenge ni bilionea wa kutupwa ambaye kwake shilingi Bilioni moja anayodaiwa kuificha huko Marekani ni sawa na "vijisenti" vichache. Hivi tatizo letu liko wapi? Je yawezekena kuwa chenge ni dalili tu ya tatizo? Je eye ni kiongozi pekee wa TAnzania ambaye amewekeza mabilioni ya shilingi kwenye akaunti za kigeni? Je ajiuzulu au na yeye anaweza akalia kuwa amefanywa "Bangusilo" wa rada!? Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website KLH Exclusive: "Mafuriko Kyela - 40,000 hatarini!" - Dr. Harrison MwakyembePichani baadhi ya wananchi wakijaribu kuvuka mto. Kidaraja hicho sasa hakipitiki tena. Picha kwa hisani ya Mjengwa
Mvua za masika zimezidi kupamba moto nchini na zimekuwa zikisababisha mafuriko sehemu mbalimbali. Baadhi ya maeneo ambayo yamepata mafuriko ni pamoja na Vunjo, Same na Kyela. Hata hivyo hadi hivi sasa ni wilaya ya Kyela ambayo ina kata 15 ambazo kati ya hizo 11 zimepatwa na mafuriko makubwa .
Siku ya Jumamosi nimepata nafasi ya kuzungumza na Mbunge wa Jimbo la Kyela Dr. Harr ... Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Bila CCM Madhubuti? - Mwalimu alisema kweli...Mwanzoni sikuyaelewa maneno ya Baba wa Taifa Mwl. J.K. Nyerere kuwa “Bila CCM Madhubuti nchi yetu itayumba”. Nilifirikia kuwa alimaanisha “Bila CCM” nchi yetu itayumba, na pia nilidhania alimaanisha kuwa “Bila viongozi wa CCM” nchi yetu itayumba. Miaka hii ilivyopita na hasa baada ya matukio yaliyolikumba Taifa letu ndio maana hasa ya maneno yake imeanza kuniingia na kwa hakika nimekubali kuwa bila Chama cha Mapinduzi ambacho ni “madhubuti” basi Taifa letu liko matatani, na kwa hakika lita ... Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Operesheni Demokrasia Comoro - Wangwe angekaa kimya!Saa na wakati huu vikosi vya majeshi ya Jumuiya ya Afrika vimeanza mapambano ya kukikomboa kisiwa cha Anjouan ili hatimaye kurudi katika shirikisho la Comoro. Vikosi hivyo vikiongozwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania wanashiriki katika Operesheni Demokrasia Komoro yenye lengo la kumuondoa Rais aliyejipachika Bw. Mohammed Bacar.
Hivyo saa na wakati kama huu ambapo vijana wetu wako katika hali ya hatari na ambapo wanayaweka maisha yao hatarini ni kitendo cha kutokuwajibika kwa mwanasiasa kam ... Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Sisi tumepotea wapi?Ndugu zangu, mlolongo wa matukio ambayo yameliandama Taifa letu kwa miaka kadhaa sasa na ambayo kilele chake bado hatujui kitafikia lini yanathibitisha jambo moja kubwa, kwamba sisi kama Taifa kuna mahali tumekwenda kombo. Kuna mahali ambapo sisi kama taifa tumepotea njia na hatuko tayari kukubali kuwa tumepotea na matokeo yake tumeendelea kufuata njia ile ile ya upotevu tukiamini kuwa huko mbeleni mambo yatanyoka.
Je, Tanzania tunayoiona leo hii, ndiyo hii ambayo tuliitaka na ambayo waze ... Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Walioiba EPA wasiepe Pingu! Habari za kuwa wale walioifanya uhalifu kwenye akaunti ya EPA wameanza kurudisha fedha zile zimepokelewa kwa hisia zinazopingana. Kuna wale ambao wanaona uamuzi huo ni wa kupongeza kuwa "angalau fedha zinarudi" na hawa wanasema kuwa baada ya fedha kurudi ndiyo tufuatilie suala la kupelekwa wahalifu hawa mahakamani.
Kuna wale wengine ambao wanaamini kuwa fedha kurudishwa kungeenda sambamba na wahalifu kuchukuliwa hatua za kisheria badala ya ilivyo sasa. Watu hawa nikiwemo mimi naamini tun ... Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Mahojiano na DCI : "Jambo Forums haihusiani na Ughaidi"Baada ya msemaji wa Jeshi la Polisi kuihusisha Jambo Forums na Ughaidi niliamua kutafuta msimamo wa wale wanaochunguza ili watuambie kweli wana amini kuwa JF inahusiana na Ughaidi.
Nilipata nafasi ya kuzungumza na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) Kamanda Robert Manumba na kumuuliza mambo kadhaa yanayohusiana na Jambo Forums na kukamatwa kwa wawili kati ya wanachama wake kama 4000.
Tafadhali karibu usikilize mahojiano hayo na kwa habarii za kutwa nzima usikose kuingia http://www.klhnew ... Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Jambo Forums na Ughaidi?Jana ilikuwa ni siku ya huzuni katika jitihada za kupanua uhuru wa habari na maoni Tanzania; jeshi la Polisi lilikiri kuwa linawashikilia watu wawili kutokana na kuhusika kwao na JF kwa madai kuwa tovuti hiyo inahusiana na uchochezi na mambo ya Kighaidi.
Inasikitisha kuona kuwa Jeshi letu la Polisi badala ya kuwakamata watu waliokwapua fedha za umma na ambao wameliingizia Taifa letu hasara limeamua kuwatafuta watu walioufunua ufisadi hadharani. Hili limesikitisha sana. Ni kwa sababu hiyo w ... Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Mizengo Pinda Waziri Mkuu mteulePichani Waziri Mkuu Mteule Bw. Mizengo Pinda akipongezwa na wabunge mara baada ya kulipitisha jina lake kuwa Waziri Mkuu
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mhe. Mizengo Pinda (Mpanda Mashariki) kuwa Waziri Mkuu mpya kuchukua nafasi ya Mhe. Edward Lowassa aliyejiuzulu kufuatia kashfa ya Richmond.
KLH News international inakuletea taarifa ya uteuzi huo hapa kwenye podomatic na pia kwenye http://www.klhnews.com ambapo tunafuatilia maendeleo ya sakata hili linalojifunua kila baada ya masaa ... Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Lowassa aandika barua ya kujiuzulu- JK atakubali?Tafadhali sikiliza maoni yangu kuhusu hili. Na zaidi ya yote hakikisha unatembelea KLH News through out the day for any breaking news and for any new development kufuatia kashfa hii ya Richmond. Ukienda kwenye "Archives" hapa utaweza kusikiliza mahojiano yangu na Dr. Mwakyembe miezi michache iliyopita.
Pichani Mbunge wa Kyela - CCM na Mwenyekiti wa Kamati iliyochunguza Richmond Mhe. Dr. Harrison Mwakyembe akitopewa mkono wa pongezi (pole?) na wabunge wenzake. Picha kwa hisani ya Mroki Mro ... Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Wabunge wanaokurupuka, na Kampeni za KitetoLeo hii vichwa vya habari vya magazeti mengi nyumbani vinahusu jinsi wabunge walivyodai ripoti kamili ya uchunguzi wa BoT badala ya maelezo ya juu yaliyotolewa na Waziri wa Fedha Bi. Zakia Meghji Bungeni jana.
Binafsi siyo tu nasikia kinyaa lakini nakerwa na wabunge ambao kama watu walioamshwa usingizini wanakurupuka na kuanza kujifanya ati leo wamekuwa watetezi wa BoT
Wabunge hawa walikuwa wapi wakati wa miaka 15 ya ufisadi kwenye benki yetu Kuu? Walikuwa wapi wakati Meremeta na ndugu za ... Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Tumepigwa ganzi ya Ufisadi?Mlolongo wa kashfa umeigubika serikali ya Tanzania na kama vile watu wanashindana imekuwa ni kashfa juu ya kashfa.
Swali ambalo linanisumbua hasa baada ya kashfa ya BoT naona watu wamekuwa kama wametiwa ganzi ya aina fulani, kuwa hatusikii tena uchungu na tumekubali kuwa "mambo ndivyo yalivyo"
Je tukubali kuwa tuko katika utamaduni wa kifisadi na mambo ndivyo yalivyo? Je tukubali kuwa sisi sote ni mafisadi wa aina moja au nyingine na tukipewa nafasi hizo walizonazo wao bila ya shaka na ... Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Mahojiano na Waziri wa Fedha Bi. Zakia Meghji (MB)Je, Bi. Zakia Meghji naye ni fisadi? Je kitendo chake cha kuandika barua kuthibitisha malipo kwa kampuni iliyotajwa kwenye ripoti ya BoT na baadaye kuikana barua hiyo baada ya kufahamu ukweli ni kitendo cha kifisadi? Je, anapaswa kujiuzulu?
Nimezungumza na waziri wetu wa fedha kujaribu kutafuta baadhi ya majibu ya maswali hayo. Sikiliiza na uamue mwenyewe. Kama huwezi kusikiliza hapa kwa sababu yeyote ile, unaweza kusikiliza mahojiano haya kwenye http://www.klhnews.com eneo la podcast pal ... Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Ripoti ya Kamati Teule kuhusu Richmond, wananchi wasubiri! Hatimaye Ripoti ya uchunguzi kuhusu kampuni ya Richmond Development ya Houston imekamilika na hatimaye kukabidhiwa rasmi kwa Spika wa Jamhuri ya Muungano hapo jana na Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge Dr. Harrison Mwakyembe (Kyela - CCM) pichani.
Kamati hiyo imetumia siku 45, mashahidi 75, vielelezo zaidi ya mia moja na maswali zaidi ya 2700. Kwa kifupi ni kuwa ukilinganisha na uchunguzi wa PCCB inawezekana wananchi watataka Kamati Teule ifanye uchunguzi wa mambo mengine yote kuliko Taas ... Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Heri ya Krismasi !Wapendwa wasikilizaji kwa niaba yangu na ya KLH News napenda kuwatakia ndugu zetu Wakristu mahali pote duniani na wengine wote heri ya Krismasi wanapoadhimisha kuzaliwa kwa Mkombozi Bwana Yesu Kristu. Kutoka hapa kijijini na kwenu nyote nawatakia heri ya Krismasi. Mnayoisikiliza ni kwaya ya Vijana ya Kanisa Katoliki la Mtakatifu Theresa Arusha mjini. Albamu yao inatoka hivi karibuni na bila ya shaka kwa watakaopenda wanaweza kuwasiliana nami kuona jinsi gani wataweza kuinunua. Listen | Listen in your iPhone | Download | View full cache | Visit Website Eid Mubarak!Napenda kutumia nafasi hii kuwatakia heri ya siku kuu ya Eid ndugu zetu waislamu wanapoungana na na Waislamu wengine katika kuunganisha mioyo yao katika kuhitimisha mojawapo ya Nguzo za Uislamu, yaani Hijja. Tunapowafikiria wale waliokuwa wamekwama uwanja wa ndege tuna matumaini kuwa serikali imefanya mipango mizuri na ya uhakika ili kuweza kuwarudisha wote salama na bila ya usumbufu wowote ule. Listen | Listen in your iPhone | Download | |