Link to the Show / Show Notes
Aliyewahi kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dr. Daud Balali amefariki dunia. Habari ambazo zimeanza kusikika tangu jana jioni na kuthibitishwa na ndugu zake zimesema kuwa Gavana Balali amefariki mwishoni mwa juma na mipango ya mazishi inafanywa. Anatarajiwa kuzikwa huko huko Marekani. Inatarajiwa taarifa ya kifo chake kutangazwa Tanzania baadaye leo. Sikiliza matangazo kuhusu kifo hicho hapa au kwa kutwa nzima ya kesho tutakuwa tunaleta maendeleo yoyote ya habari hii kwenye tovuti yetu ya http://www.klhnews.com ambako "we bring the news first".

Play in your Iphone